Luke 4:16-21

16 aIsa akaenda Nasiri, alipolelewa, na siku ya Sabato alikwenda katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake. Akasimama ili asome, 17 bnaye akapewa kitabu cha nabii Isaya, akakifungua na kukuta mahali palipoandikwa:
18 c“Roho wa Bwana yu juu yangu,
kwa sababu amenitia mafuta
kuwahubiria maskini habari njema.
Amenituma kuwatangazia wafungwa
kufunguliwa kwao,
na vipofu kupata kuona tena,
kuwaweka huru wanaoonewa,

19 na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubalika.”

20 dKisha akakifunga kitabu, akamrudishia mtumishi na akaketi. Watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. 21 eNdipo akaanza kwa kuwaambia, “Leo Andiko hili limetimia mkiwa mnasikia.”

Copyright information for SwhKC